Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika MkutanoMkuu wa 39 wa Mwaka wa Mamlaka ya Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT)utakaofanyika Machi 11-12, 2025 jijini Dodoma katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Mhe.Murshid Ngeze amesema mkutano huo ni wa kawaida ambao hufanyika kila mwaka,ambapo pamoja na mambo mengine, utajadili masuala mbalimbaliyanayoendelea katika serikali za mitaa na utafanya tathmini ya mipango na mikakati ya ALAT
Mhe.Ngeze amesema mkutano huo utahudhuriwa pia na wageni kutoka ndani na nje ya nchi. Amesema Katibu wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Afrika Mashariki na mabalozi kutoka mataifa ya nje nao wanatarajiwa kuhudhuria katika mkutano huo.
Mhe.Ngeze ametumia nafasi hiyo pia kuwakaribisha kuhudhuria mkutano huo wajumbe wa mkutano huo akiwataja wajumbe hao kuwa ni wakurugenzi wa halmashauri zote nchini, Mameya wa halmashauri zote nchini, Wenyeviti wa halmashauri zote nchini na wabunge (katika kila mkoa mbunge mmoja) pia amewaalika pia wananchi kufuatilia matangazo ya mkutano huo kupitia vyombo vya habari mbalimbali vitakavyorusha matangazo hayo moja kwa moja kutoka jijini Dodoma
Jengo la Sokoine,Barabara ya CDA Dodoma
Postal Address: P.O.Box 2049 DODOMA
Telephone: 0262323407
Mobile: +255(0)784209840 au
Email: alat_tz@yahoo.com
Copyright ©2018 ALAT . All rights reserved.