Na Mwandishi wetu, Dodoma
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Mhe. Murshid Hashim Ngeze, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa juhudi kubwa inazochukua katika kuboresha huduma za kijamii na kuendeleza miradi mikubwa inayofaidisha wananchi.
Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 39 wa ALAT uliofanyika tarehe 11 Machi, 2025 katika Ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete Convention, Jijini Dodoma, Mhe. Ngeze ametaja mafanikio mengi yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia SuluhuHassan.
Ameeleza kuwa miradi mikubwa kama reli ya kisasa (SGR), bwawa la Mwl. Julius Kambarage Nyerere, na miundombinu mingine imechangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania, na kwamba miradi hii inatoa fursa nyingi za ajira namaendeleo kwa jamii.
Aidha, Mhe. Ngeze amesisitiza umuhimu wa miradi hiyo katika kuongeza ufufuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi, akisema kuwa hatua hizo zinaonyesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi.
Ameongeza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya uongozi thabiti wa Rais Samia na juhudi zake za kuhakikisha kuwa miradi mikubwa inatekelezwa kwa ufanisi, ikilenga kuboresha huduma za kijamii na kuleta maendeleo endelevu katika maeneo yote ya nchi.
Mhe. Ngeze amesema ALAT imeendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi, ikiwa ni pamoja na usimamizi wa wanachama wake, uwakilishi wa maslahi ya Serikali za Mitaa kimataifa, na kutoa huduma bora kwa wananchi kupitia mafunzo na usambazaji wa habari muhimu.
Amepongeza Serikali kwa kutenga fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta za afya, elimu, barabara,na kilimo, na kuongeza kuwa juhudi hizi zimeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya Watanzania.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kushirikiana kwaumoja na uadilifu katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2025, akitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuchagua viongozi bora kwa ajili ya maendeleo endelevu ya nchi.
Mhe. Ngeze ameishukuru Serikali kwa msaada mkubwa katika maandalizi ya mkutano huo, na kutoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, kwa ushirikiano wake mkubwa.
Jengo la Sokoine,Barabara ya CDA Dodoma
Postal Address: P.O.Box 2049 DODOMA
Telephone: 0262323407
Mobile: +255(0)784209840 au
Email: alat_tz@yahoo.com
Copyright ©2018 ALAT . All rights reserved.