JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA
(ALAT).
1: |
ALAT ni nini?
|
|
ALAT ni kifupi cha "Association of Local Authorities of Tanzania" ambacho kwa kiswahili ni Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania. Jumuiya hii ilianzishwa tarehe 13 Desemba, 1984 mara baada ya kurejeshwa kwa Mfumo wa Serikali za Mitaa kwa Sheria Na. 7 na 8 za mwaka 1982.
|
|
Kwa hiyo, ALAT ni Jumuiya ya Halmashauri zote za Wilaya na za Miji, Miji Midogo na Vijiji Tanzania Bara. Halmashauri za Miji ni pamoja na Majiji, Manispaa na Halmashauri za Miji. Aidha, Halmashauri za Wilaya hujumuisha pia Serikali za Vijiji.
|
2: |
Majukumu ya Jumuiya
|
|
Majukumu ya msingi ya Jumuiya hii kwa mujibu wa Katiba yake ni: usimamizi, uwakilishi, utetezi, ushawishi na utoaji huduma:
|
|
Usimamizi |
|
ALAT ina jukumu la kusimamia kuwa wanachama wake wanatekeleza wajibu kwa mujibu wa sheria zao.
|
|
Uwakilishi:
|
|
Kwa jukumu hili Jumuiya hii huziwakilisha Serikali za Mitaa katika mikutano ya kitaifa na kimataifa inayohusu Serikali za Mitaa. Aidha, ni jukumu lake pia kuwasilisha Serikalini maoni na mapendekezo ya Serikali za Mitaa kuhusu jambo lolote ambalo linaonekana ni la manufaa kwa wananchi.
|
|
Utetezi
Kwa jukumu la utetezi ALAT hutetea haki na maslahi ya Serikali za Mitaa na huchukua kila hatua za lazima kuhakikisha kuwa haki na maslahi hayo yanalindwa. |
|
Ushawishi
|
|
Kwa ushawishi ALAT inawashawishi watunge sera ama Watunga Sheria (Wabunge) kupitisha sera ama sheria kwa kuwa zina manufaa kwa Serikali za Mitaa au ina washawishi wahusika wasizipitishe kwa kuwa zinaathiri Serikali za Mitaa.
|
|
Utoaji huduma
|
|
Jukumu la ALAT la kutoa huduma kwa Halmashauri ni pamoja na kutafuta na kupata habari, ushauri na maoni ya kitaalam kuhusu serikali za mitaa na kuyasambaza kwa wanachama. Huduma nyingine ni pamoja na utoaji wa mafunzo ya ujengaji uwezo kwa Madiwani na Watendaji wao, ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
|
|
Usambazaji wa habari
|
|
Jukumu lingine la ALAT ni kusambaza habari zozote muhimu zihusuzo Serikali za Mitaa kwa Halmashauri wanachama na umma kwa jumla kwa njia ya nyaraka, radio na makala na kwa Jarida la ALAT n.k. Kwa njia hii. Halmashauri zinaweza pia kupashana habari na kubadilishana uzoefu juu ya shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Halmashauri zao hususan kuhusu mifano bora ambayo inafaa kuigwa.
|
Jengo la Sokoine,Barabara ya CDA Dodoma
Postal Address: P.O.Box 2049 DODOMA
Telephone: 0262323407
Mobile: +255(0)784209840 au
Email: alat_tz@yahoo.com
Copyright ©2018 ALAT . All rights reserved.