• complaint |
    • Wasiliana nasi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
ASSOCIATION OF LOCAL AUTHORITIES OF TANZANIA-ALAT
ASSOCIATION OF LOCAL AUTHORITIES OF TANZANIA-ALAT

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania

  • Home
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Mission and Vision
  • Tunafanya nini?
    • Service one
    • Services two
  • Utawala
    • Organization Structure
  • Machapisho
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Utawala
    • Application Forms
  • Kituo cha Habari
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Habari Mpya
    • Matukio
  • Projects
    • lic projects
  • Halmashauri

NMB Yadhamini Mkutano Mkuu wa 39 wa ALAT kwa Sh Milioni 170

Posted on: March 10th, 2025

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Benki ya NMB imetoa Jumla ya Sh170 milioni kama sehemu ya udhamini wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT).Kiasi hicho ni sehemu ya jumla ya fedha Sh1.4 bilioni zilizokwishakutolewa na benki hiyo kwa ajili ya ALAT katika kipindicha miaka 9 tangu NMB ilipoanza kuwadhamini.

Mkutano huo utafanyika Jijini Dodoma kuanzia kesho Machi 11,2025 ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan.

Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali Bw. Alfred Shao, amekabidhi hundi kwa uongozi wa ALAT leo Machi 10,2025 huku akisisitiza kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana na chombo hicho kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.

Bw.Shao amesema ndani ya kipindi hicho wamepata ushirikiano wa kutosha kutoka ALAT na hivyo hawaoni shida ya kuendelea kuwadhamini na kwamba wanafanya hivyo kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.

“Pamoja na kiasi hiki, itakumbukwa tulianza kutoa mchango wetu karibu miaka 9 iliyopita na hadi leo tutakuwa tumefikisha Jumla ya Sh1.4 bilioni,tunaamini mashirikiano haya tutayaendeleza,” amesema Bw.Shao.

Afisa huyo amesema fedha walizokabidhi kwa leo, Jumla ya Sh100 milioni zinatolewa kama fedha taslimu wakati Sh70 milioni zinatolewa kama vifaa na huduma zingine.

Hata hivyo amewakaribisha wajumbe wote wa ALAT kushirikiana na benki hiyo katika ibada ya futari itakayofanyika kesho Jumanne Machi 11,2025 iliwajumuike kwa pamoja na kupata muda wa kubadirishana mawazo huku akisisitiza kuwa, katika kipindi chote cha Mkutano huo NMB wataendelea kutoa huduma zao katika banda lao lililopo katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center (JKCC).

Mwenyekiti wa ALAT Mhe.Murshid Ngeze amesema yapo mengi ambayo chombo hicho kinajivunia baada ya kuanzisha ushirikiano na NMB lakini kikubwa ni jinsi Benki hiyo ilivyowarahisishia huduma kwa wananchi wao.

Mhe.Ngeze amesema hawajawahi kukwama jambo lolote katika kuwahudumia wananchi kupitia Halmashauri huko vijijini baada ya NMB kufika karibu maeneoyote na kurahisisha upatikanaji wa huduma.

“Asubuhi nilikuwa kwenye kipindi kimoja na TV fulani (anaitaja) waliniuliza swali kwamba sisi ALAT tunanufaikaje kuwa karibu na NMB, nimewambia vitu vingi, lakini hatujawahi kukwama kwenye huduma zetu ndani ya Halmashauri yoyote iliyojiunga na mtandao wa NMB, hakika hawa ni ndugu zetu na zaidi ya ndugu,” amesema Mhe Ngeze.

Makamu Mwenyekiti wa ALAT Mhe.Sima Constantine amesema hakuna kitu wala jambo linaloweza kuwazuia kuwa na ushirikiano na NMB kwani mara nyingi wamekuwa wakipata mafanikio makubwa ndani ya benki hiyo.

Matangazo

  • MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI. March 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Rais Samia Aziagiza Halmashauri Kusimamia Mapato na Matumizi Sahihi

    March 13, 2025
  • ALAT yaipongeza Serikali kwa Maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa

    March 11, 2025
  • Waziri Mchengerwa awataka Viongozi wa Mitaa kusukuma maendeleo katika maeneo yao

    March 12, 2025
  • NMB Yadhamini Mkutano Mkuu wa 39 wa ALAT kwa Sh Milioni 170

    March 10, 2025
  • View All

Video

mikumi
More Videos

Quick Links

  • ALAT

Related Links

  • TAMISEMI
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Jengo la Sokoine,Barabara ya CDA Dodoma

    Postal Address: P.O.Box 2049 DODOMA

    Telephone: 0262323407

    Mobile: +255(0)784209840 au

    Email: alat_tz@yahoo.com

Mawasiliano mengine

   

Wanaotembelea

Visitors Counter

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2018 ALAT . All rights reserved.