• complaint |
    • Wasiliana nasi |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
ASSOCIATION OF LOCAL AUTHORITIES OF TANZANIA-ALAT
ASSOCIATION OF LOCAL AUTHORITIES OF TANZANIA-ALAT

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania

  • Home
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Mission and Vision
  • Tunafanya nini?
    • Service one
    • Services two
  • Utawala
    • Organization Structure
  • Machapisho
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Utawala
    • Application Forms
  • Kituo cha Habari
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Habari Mpya
    • Matukio
  • Projects
    • lic projects
  • Halmashauri

Makamu wa Rais Kufungua Mkutano Mkuu wa ALAT Arusha

Posted on: May 28th, 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kesho atakuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) utakaofanyika katika Ukumbi wa Simba AICC jijini Arusha.

Mkutano huo utakaofanyika kuanzia tarehe 29 Mei, 2023 na kukamilika tarehe 31 Mei, 2023 utawakutanisha washiriki 600, wakiwemo Wastahiki Mameya wa Majiji na Manispaa, Waheshimiwa Wenyeviti wa Halmashauri, na Wakurugenzi wa Halmashauri zote 184  za Tanzania Bara.

Kaimu Katibu Mkuu wa ALAT Taifa Bw. Mohamed Maje amesema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya kufanyika kwa mkutano huo yamekamilika.

Wakati huo huo, Benki ya NMB leo tarehe 28 Mei, 2023, imekabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya kufanikisha Mkutano Mkuu wa 37 wa ALAT.

Hafla hiyo fupi ilihudhuriwa na Viongozi wa ALAT Taaifa wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mhe. Sima Constantine Sima, Katibu Mkuu wa ALAT Bw. Mohamed Maje, na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Tendaji wa Jumuiya hiyo.

Akizungumza kabla ya kupokea hundi  hiyo, Makamu Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mhe. Sima Constantine Sima ameishukuru Benki ya NMB kwa kushirikiana na Jumuiya hiyo kwa muda wa miaka 7

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB Bw. Alfred Shao ambaye alimwakilisha Mtendaji Mkuu wa NMB amesema Benki hiyo na ALAT wamekuwa wakishirikiana pamoja katika kuboresha miundombinu ya Elimu, Afya, Usafiri na Mazingira kupitia halmashauri 184 nchini.

Amesema Benki ya NMB imeendelea kuboresha huduma zake  ili kuweza kuhudumia Serikali Kuu pamoja na Serikali za Mitaa.

Ameongeza kuwa kazi kubwa ya Benki hiyo ni ni kurahisisha makusanyo ya kodi kupitia mifumo bora inayowezesha Serikali ya awamu yaa ssita katika makusanyo ya mapato.

 

 

Matangazo

  • MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI. March 17, 2022
  • View All

Latest News

  • Rais Samia Aziagiza Halmashauri Kusimamia Mapato na Matumizi Sahihi

    March 13, 2025
  • ALAT yaipongeza Serikali kwa Maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa

    March 11, 2025
  • Waziri Mchengerwa awataka Viongozi wa Mitaa kusukuma maendeleo katika maeneo yao

    March 12, 2025
  • NMB Yadhamini Mkutano Mkuu wa 39 wa ALAT kwa Sh Milioni 170

    March 10, 2025
  • View All

Video

mikumi
More Videos

Quick Links

  • ALAT

Related Links

  • TAMISEMI
  • NECTA

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Jengo la Sokoine,Barabara ya CDA Dodoma

    Postal Address: P.O.Box 2049 DODOMA

    Telephone: 0262323407

    Mobile: +255(0)784209840 au

    Email: alat_tz@yahoo.com

Mawasiliano mengine

   

Wanaotembelea

Visitors Counter

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2018 ALAT . All rights reserved.