Wednesday 22nd, January 2025
@ARUSHA
ZIARA YA KATIBU MKUU – ALAT KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA MACHI 11, 2022.
Katibu Mkuu – ALAT alifanya ziara katika Halmashauri ya Jiji la Arusha Machi 11, 2022 ikiwa ni muendelezo wa ziara zilizofanywa katika Mikoa mbalimbali. Kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu, fedha za mapato ya ndani na fedha za UVIKO katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Miradi iliyokaguliwa Katika Halmashauri ya Jiji la Arusha ni pamoja na Shule ya Sekondari Arusha, ambapo Halmashauri hiyo ilipokea kiasi cha Shilingi Bilioni 2.1 na wamefanikiwa kujenga vyumba 105 vya madarasa.
“apongeza jitihada zilizochukuliwa katika Ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa vya ghorofa, na kuzitaka Halmashauri zote Nchini kuiga mfano huo kutokana na ufinyu wa maeneo, na kuzitaka Halmashauri kuachana na Holizontal Development na kwenda kwenye Vertical Development kwa maana ya kwamba swala la kutandaza majengo tuachane nalo”.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu ALAT ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Arusha ambapo alikagua Jengo la upasuaji, Jengo la Wagonjwa wa nje OPD. Pia, amekagua mradi wa Ujenzi wa Hospitali mpya ya Kitalii inayojengwa na Halmashauri hiyo (Tourist Hospital) ambapo maandalizi ya Ujenzi huo yameanza.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu ALAT, ampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kupata mkopo wenye masharti nafuu wa Shilingi Trilioni 1.5 kutoka Benki ya Dunia, fedha zilizoelekezwa katika Ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa Nchi nzima. Kwa namna maandiko na ushawishi uliyotumika kuonyesha jinsi gani madarasa hayo yatapunguza maambukizi ya Ugonjwa wa Uviko na ikizingatiwa ya kwamba Tanzania haikuweza kusitisha shughuli za kijamii kama ilivyokuwa katika Mataifa mengine (Lockdown).
Katibu Mkuu alidhishwa na Miradi yote aliyotembelea kwa kuona thamani ya fedha iliyotumika (Value for Money) kutokana na makusanyo ya fedha za ndani na fedha kutoka Serikali kuu.
Wasalaam.
Jengo la Sokoine,Barabara ya CDA Dodoma
Postal Address: P.O.Box 2049 DODOMA
Telephone: 0262323407
Mobile: +255(0)784209840 au
Email: alat_tz@yahoo.com
Copyright ©2018 ALAT . All rights reserved.