Wednesday 18th, September 2024
@MWANZA GEITA
MWENYEKITI NA KATIBU MKUU – ALAT WAFANYA ZIARA KATIKA MIKOA YA MWANZA NA GEITA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.
Mwenyekiti na Katibu Mkuu – ALAT walifanya ziara katika Halmashauri za Mikoa ya Mwanza na Geita. Kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu, fedha za mapato ya ndani na fedha za UVIKO katika ujenzi wa vyumba vya madarasa. Pia kuimarisha ALAT na Matawi yake:- Kutembelea Matawi ya ALAT ya Mikoa, Halmashauri na Kata.
Katika hatua nyingine, Miradi yote ilikaguliwa Katika Halmashauri za Mikoa ya Mwanza na Geita, na kujiridhisha juu ya utekelezaji wake kwa kuona thamani ya fedha iliyotumika (Value for Money) kutokana na makusanyo ya fedha za ndani na fedha kutoka Serikali kuu. Halmashauri zilihamasishwa juu ya ulipaji wa madeni na michango ya Jumuiya ili kufanikisha maandalizi ya Mkutano Mkuu wa 36 wa ALAT TAIFA utakaofanyika Jijini Mbeya Mei 2022 na uendeshaji wa shughuli za ALAT.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa ALAT TAIFA alitoa maelekezo kuhusu gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 lililonunuliwa na Halmashauri hiyo kupitia mapato yake ya ndani liweze kurejeshwa katika Halmashauri ya Mji wa Geita kwani lilichukuliwa na kupelekwa Serikali Kuu na hakuna taarifa yoyote kuhusu gari hilo.
Pia, Mwenyekiti na Katibu Mkuu ALAT walishiriki katika Mkutano Mkuu wa Ushirikiano wa Halmashauri zinazozunguka Ukanda wa Ziwa Victoria (LVRLAC) Tarehe 24 - 25 February 2022 Jijini Mwanza.
Wasalaam.
Jengo la Sokoine,Barabara ya CDA Dodoma
Postal Address: P.O.Box 2049 DODOMA
Telephone: 0262323407
Mobile: +255(0)784209840 au
Email: alat_tz@yahoo.com
Copyright ©2018 ALAT . All rights reserved.