Thursday 10th, October 2024
@ARUSHA
Mwenyekiti wa ALAT TAIFA Mhe. Murshid Ngeze, alipata mwaliko wa kuhudhuria Kikao cha Jumuiya ya Serikali za Mitaa Afrika, kikao kilichofanyika Machi 07 – 08, 2022, Nairobi Kenya. Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ni mwanachama wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Afrika (UCLG).
Mwaliko huo ulijumuisha Katibu Mkuu ALAT TAIFA, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke na Mwenyekiti wa WASEMI TAIFA.
Jumuiya ya Serikali za Mitaa Afrika hufanya vikao vyake vya kawaida kwa kuzingatia Katiba ya (UCLG). Kikao hicho kiliJjadili maswala mbalimbali ya Serikali za Mitaa kikanda, Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Afrika pamoja na mambo mengine ya kiutendaji ya UCLG yanayohusu ustahimilivu, mikakati na malengo ya Jumuiya ya Serikali za Mitaa Afrika.
Aidha jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), itaendelea kuwa Mwanachama wa UCLG (United Cities and Local Government of Africa) kwa kuzingatia Mkataba wa Umoja wa Afrika na sera zetu za mambo ya Nje.
Wasalaam.
Jengo la Sokoine,Barabara ya CDA Dodoma
Postal Address: P.O.Box 2049 DODOMA
Telephone: 0262323407
Mobile: +255(0)784209840 au
Email: alat_tz@yahoo.com
Copyright ©2018 ALAT . All rights reserved.