Wednesday 22nd, January 2025
@ARUSHA
Mwenyekiti wa ALAT TAIFA Mhe. Murshid Ngeze, alipata mwaliko wa kuhudhuria Kikao cha Jumuiya ya Serikali za Mitaa Afrika Mashariki, kikao kilichofanyika Jijini Arusha. Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ni mwanachama wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Afrika Mashariki (EALGA).
Mwaliko huo ulijumuisha Mjumbe Mmoja wa Kamati ya Utendaji katika nafasi ya Wanawake ambapo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Mhe. Yagi Maulid Kiaratu aliweza kuwakilisha pamoja na Katibu Mkuu ALAT.
Jumuiya ya Serikali za Mitaa Afrika Mashariki hufanya vikao vyake vya kawaida kwa kuzingatia Katiba ya (EALGA). Kikao hicho kilikuwa ni cha Kamati ya Utendaji ya EALGA kilichojadili maswala mbalimbali yanayohusu ustahimilivu, mikakati na malengo ya Jumuiya ya Serikali za Mitaa Afrika Mashariki.
Aidha jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), itaendelea kuwa Mwanachama wa EALGA (East Africa Local Governments Association) kwa kuzingatia Misingi ya Mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Wasalaam.
Jengo la Sokoine,Barabara ya CDA Dodoma
Postal Address: P.O.Box 2049 DODOMA
Telephone: 0262323407
Mobile: +255(0)784209840 au
Email: alat_tz@yahoo.com
Copyright ©2018 ALAT . All rights reserved.